Picha · Ramani · Gharama
Ona nyumba yako ya vyumba vitatu kabla ya kujenga
Chagua ramani ya vyumba vitatu yenye vipimo, ona picha za nyumba kwa pande zote na upate makadirio ya gharama, yote kwenye simu yako.
Ushauri wa bure
Kabla ya kujenga
Hakiki kiwanja
Hakikisha kiwanja kimepimwa na hati ni halali. Fanya upekuzi (search) ofisi ya ardhi kabla ya kulipa.
Chagua ramani
Linganisha ukubwa wa nyumba na kiwanja. Acha nafasi ya mipaka, maegesho na tanki la maji taka.
Omba kibali cha ujenzi
Michoro ya kibali inahitaji muhuri wa mbunifu aliyesajiliwa. Wasilisha halmashauri ya eneo lako.
Panga bajeti
Tumia makadirio ya gharama kupanga fedha za kila hatua. Jenga kwa hatua kulingana na fedha ulizonazo.
Maswali
Maswali kuhusu ramani ya vyumba vitatu
Ramani ya vyumba vitatu inagharimu kiasi gani?
Ramani pamoja na picha ni TZS 5,000. Kifurushi kamili chenye makadirio ya gharama za ujenzi ni TZS 15,000. Unalipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa, kisha unapakua PDF papo hapo.
Nyumba ya vyumba vitatu inahitaji kiwanja cha ukubwa gani?
Ramani zetu zinafaa viwanja vya 15 × 20 m, 20 × 20 m, 20 × 25 m. Ndogo kuliko zote ni VV-2 (85 m²), inayofaa kiwanja cha 15 × 20 m.
Gharama ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu ni kiasi gani?
Inategemea ukubwa wa nyumba, udongo wa kiwanja, bei za vifaa na ubora wa finishing. Kifurushi kamili cha TZS 15,000 kinakupa makadirio ya ramani uliyochagua, kwa kila hatua na kwa kila kifaa.
Ramani hii inatosha kupata kibali cha ujenzi?
Hapana. Hii ni ramani ya awali, wazo la kuanzia. Kwa kibali cha ujenzi, ramani ichorwe kikamilifu na kupigwa muhuri na mbunifu aliyesajiliwa, kisha iwasilishwe halmashauri ya eneo lako.
PDF ya ramani ina nini?
Ramani yenye vipimo vya kila chumba na picha za nyumba. Kifurushi kamili kinaongeza gharama kwa kila hatua (msingi, boma, paa na finishing) na orodha ya vifaa kama tofali, mabati na saruji.
Chumba cha self (self contained) ni nini?
Ni chumba cha kulala chenye choo na bafu ndani yake, kinachoitwa pia master. Kila ramani yetu ina chumba kimoja cha aina hii.
Naweza kubadilisha ramani ili ifae kiwanja changu?
Ndiyo. Ramani yetu ni mwanzo; mbunifu aliyesajiliwa anaweza kuibadilisha ili ifae kiwanja na mahitaji yako. Sisi si wajenzi wala wakandarasi.