Chagua Ramani

Kuhusu sisi

Kuhusu Vyumba Vitatu

Tunakusaidia kuanza safari ya nyumba yako ya vyumba vitatu: kuona, kulinganisha na kupanga mapema, kabla ya kutumia fedha nyingi.

Tunachokupa

Wazo kamili la kuanzia

  • Ramani za awaliMpangilio wa vyumba wenye vipimo.
  • Picha za nyumbaPicha za kila nyumba kutoka pande tofauti, pamoja na mwonekano wa ndani kutoka juu.
  • Makadirio ya gharamaGharama kwa kila hatua: msingi, boma, paa na finishing.
  • Ushauri wa bureHatua muhimu za kufuata kabla ya kuanza ujenzi.

Ahadi yetu

Unachoweza kututegemea

  • Bei waziTZS 5,000 au 15,000. Hakuna gharama zilizojificha.
  • Ramani zetu wenyeweHatunakili michoro ya watu wengine.
  • Unapakua papo hapoMalipo yakithibitishwa, faili lako linapatikana mara moja.
  • Ukweli kuhusu ujenziTunakueleza wazi kile ramani yetu inaweza na isichoweza kufanya.

Sisi ni mwanzo, si nyumba ya mwisho

Ramani zetu ni wazo la kuanzia. Zinakusaidia kuona nyumba unayoitaka, kuzungumza na familia na kupanga bajeti. Kabla ya kujenga, ramani yako ichorwe kwa ukamilifu na kupitishwa na mbunifu aliyesajiliwa, na upate kibali cha ujenzi kutoka halmashauri.

Sisi si wajenzi wala wakandarasi

Hatujengi nyumba, hatusimamii ujenzi na hatutoi mafundi. Kazi yetu ni kukupa wazo, picha na makadirio, ili uanze safari yako ukiwa na mwanga.

Chagua Ramani Ona bei