Chagua Ramani

Bei

Bei ya ramani na gharama

Bei moja kwa kila ramani. Lipa kwa simu na pakua papo hapo.

Kamilisha agizo

Mtandao
Jumla ya kulipaTZS 5,000

Utapokea ombi la malipo kwenye simu yako. Weka PIN kuthibitisha.

Ramani ya awali, si ya kibali cha ujenzi. Kabla ya kujenga, ichorwe kikamilifu na mbunifu aliyesajiliwa.

Maswali

Maswali kuhusu ramani ya vyumba vitatu

Ramani ya vyumba vitatu inagharimu kiasi gani?

Ramani pamoja na picha ni TZS 5,000. Kifurushi kamili chenye makadirio ya gharama za ujenzi ni TZS 15,000. Unalipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa, kisha unapakua PDF papo hapo.

Nyumba ya vyumba vitatu inahitaji kiwanja cha ukubwa gani?

Ramani zetu zinafaa viwanja vya 15 × 20 m, 20 × 20 m, 20 × 25 m. Ndogo kuliko zote ni VV-2 (85 m²), inayofaa kiwanja cha 15 × 20 m.

Gharama ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu ni kiasi gani?

Inategemea ukubwa wa nyumba, udongo wa kiwanja, bei za vifaa na ubora wa finishing. Kifurushi kamili cha TZS 15,000 kinakupa makadirio ya ramani uliyochagua, kwa kila hatua na kwa kila kifaa.

Ramani hii inatosha kupata kibali cha ujenzi?

Hapana. Hii ni ramani ya awali, wazo la kuanzia. Kwa kibali cha ujenzi, ramani ichorwe kikamilifu na kupigwa muhuri na mbunifu aliyesajiliwa, kisha iwasilishwe halmashauri ya eneo lako.

PDF ya ramani ina nini?

Ramani yenye vipimo vya kila chumba na picha za nyumba. Kifurushi kamili kinaongeza gharama kwa kila hatua (msingi, boma, paa na finishing) na orodha ya vifaa kama tofali, mabati na saruji.

Chumba cha self (self contained) ni nini?

Ni chumba cha kulala chenye choo na bafu ndani yake, kinachoitwa pia master. Kila ramani yetu ina chumba kimoja cha aina hii.

Naweza kubadilisha ramani ili ifae kiwanja changu?

Ndiyo. Ramani yetu ni mwanzo; mbunifu aliyesajiliwa anaweza kuibadilisha ili ifae kiwanja na mahitaji yako. Sisi si wajenzi wala wakandarasi.